Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KAMATI ya waamuzi Nchini imewashusha waamuzi Rajab Mrope na Ahmada Seif kutoka ligi kuu mpaka ligi daraja la kwanza.

Katika ratiba ya ligi kuu iliyotoka waamuzi hao hayakuwepo majina yao, na rasmi sasa yameonekana kwenye ratiba ya ligi daraja la kwanza.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi (kamati ya masaa 72) kuwaondoa kwenye ratiba ya ligi kuu na shauri lao kulirudisha kwenye kamati ya waamuzi.

Mrope aliondolewa kwenye ratiba hiyo baada ya kuonyesha udhaifu kwenye mechi ya Mbeya City dhidi ya Yanga kwa kutokuwa na maamuzi sahihi kwa kulikubali goli, kuliktaa na mwisho kulikubali tena mechi iliyomalizika kwa Mbeya City kushinda 2-1.

Ahmada Seif aliondolewa kwa kosa la kutokuhimili mchezo wa African Lyon dhidi ya Mbao Fc kwa kutoa penati iliyozua utata kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa Lyon kushinda 3-1.

Kamati ya waamuzi bado haijatoa maamuzi ya Mwamuzi Martin Saanya na Samuel Mpenzu ambao nao pia waliondolwa kwenye ratiba ya ligi kuu Vodacom..


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...