Karibu katika Soko la Wazi yaani Mkulima Market litakalofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mkabala na UDASA Club. Ufungaji wa mabanda utafanyika Jumatano tarehe 21 Desemba 2016 kuanzia saa 3 asubuhi hadi 12 jioni. Siku ya ufungaji wa mabanda kutakuwa na mauzo ya bidhaa mbalimbali hususani mbogamboga na matunda kutoka Muheza.

Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi (22, 24 na 24 Desemba 2016) kuanzia saa 3 asubuhi hadi 12 jioni ndio siku rasmi za maonesho na mauzo ya bidhaa mbalimbali toka kwa wadau wa kilimo, uvuvi, ufugaji na uwindaji. 

Elimu kuhusu biashara, ubora na ufungashaji wa bidhaa za kilimo utatolewa kila siku za maonesho kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 7 mchana kwenye Banda Darasa. Elimu hii ni ya wazi na bure kwa kila mudhuriaji na washiriki wa Mkulima Market.

Mkulima Market ni fursa ya kupata bidhaa bora kabisa kutoka shambani kwa bei ya shambani. Sasa ni wakati muafaka wa kuwapongeza wakulima, wafugaji, wavuvi na wawindaji wa Tanzania kwa kununua bidhaa zao katika msimu huu wa sikukuu

                                Hakuna kiingilio ni BURE kabisa kwa wahudhuriaji.
Kushiriki kuuza, kuonesha, kutoa huduma au kupata taarifa zaidi
Wasiliana na Mwandaaji Vicensia Shule 0767 254 887 
Mratibu Msaidizi (Ushiriki) Steven Peter Mfuko 0718 054 169 au tuandikie kupitia mkulimamarket@gmail.com au tufuate twitter, facebook, instagram na youtube @mkulimamarket kupata updates

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...