MIFUKO ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF imeanza utekelezaji wa awali wa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni jitahada ya mifuko hiyo kwa pamoja kuunga mkono muelekeo wa serikali ya awamu ya tano wa kuwekeza kwenye uchumi wa viwanda.

Kukamilika kwa kiwanda hicho kinachotajwa kuwa kitakuwa ni kikubwa zaidi Afrika Mashariki, kutaongeza uzalishaji wa sukari wa hapa nchini ambapo zaidi ya tani laki mbili (200,000) zitakuwa zikizalishwa kwa mwaka sambamba na kutoa ajira zaidi ya 100,000 kwa hatua ya awali.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakati alipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama aliekuwa ameambatana na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango, mbali na kuipongeza mifuko hiyo, aliwahakikishia wakazo hao kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo huku akiwaahidi kuwa mradi utatoa kipaumbele zaidi kwa wakazi wa eneo hilo hususani vijana.

“Mradi huu una ushawishi mkubwa kutoka kwa Rais John Magufuli kutokana na adhma yake ya kuibadili Tanzania kuwa nchi ya viwanda na umekuja kwa wakati muafaka. Nataka huu uwe wa mfano,’’ alisema Waziri Mhagama ambae pia aliambatana na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Stephen Kebwe, Mbunge Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayosimamia utekelezaji wa mradi huo pamoja na viongozi wengine wa serikali.

Waziri Mhagama aliwaomba watekelezaji wa mradi huo kuainisha  mapema aina ya rasilimali watu watakaohitajika kwenye mradi ili waanze kuandaliwa mapema kuepuka suala la kuagiza wataalamu kutoka nje ya nchi kuja kufanya kazi ambazo zingeweza kufanywa na wataalamu wa ndani iwapo wangeandaliwa mapema.

Kwa upande wake Waziri Mpango alisema tayari serikali imeshatenga sh bilioni 17 katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya kumalizia fidia na mipaka kwa wakazi wanaoishi kwenye shamba la miwa kwa ajili ya kiwanda hicho lenye ukubwa wa ekari 63,000.

“Lengo kubwa hapa ni kuzalisha sukari itakayotuwezesha kukidhi mahitaji yetu ya ndani na kuuza nje ya nchi pamoja na bidhaa ambatano ikiwemo ethanol. Pia nitoe wito kwa vijana wa eneo hili kuhakikisha wanakuwa katika vikundi ambavyo vitawawezesha kutekeleza kwa urahisi miradi mbalimbali ikiwemo kuanzisha mashamba yatakayosaidia kuongeza malighafi kwa kiwanda hiki,’’ alisema.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (wa tatu kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakifuatilia maelezo kutoka kwa muwakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayotekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni uwezeshaji wa pamoja wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki. 
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (wa tatu kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakifuatilia maelezo kutoka kwa muwakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayotekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni uwezeshaji wa pamoja wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki. 

 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango wakikagua ujenzi wa barabara   inayoelekea sehemu ya mradi ambayo inafanyiwa ukarabati mkubwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT.
aziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakimsikiliza Mbunge Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba (kulia) ambae jimboni kwake ndipo unatekelezwa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda hicho. 
Wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo jirani na mradi.
Wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo jirani na mradi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...