Tanga, WANAFUNZI wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa kutoka vyuo Vikuu na Shule za Sekondari na Msingi kutoka Mikoa mbalimbali nchini wamekutana Tanga kujadili mambo mbali mbali yahusuyo shughuli za Umoja wa Mataifa. 

Wanafunzi hao walijadili mambo hayo yakiwemo Demokrasia na Utawala bora Barani Afrika pamoja na changamoto za Raia katika nchi zenye machafuko. Pia walijadili uchafuzi wa mazingira kwa nchi zenye viwanda na uharibifu wa mazingira ya bahari kwa baadhi ya viwanda kumwaga sumu baharini. 


Akizungumza katika kongamano hilo, Mlezi wa (YUNA) Mkoa wa Kilimanjaro, Fransiss Shelutete, amezitaka Serikali nchi za Afrika kuwachukulia hatua kali uchafuzi wa mazingira .

Mwenyekiti wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) nchini Rahim Nassir, akizungumza kwenye kongamano la vilabu vya umoja wa Mataifa lililowashirikisha wanafunzi vyuo vikuu na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga .

Wanachama wa vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakifuatilia kongamano lililohusisha wanafunzi wa vyuoni na Shule za Sekondari na Msingi na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Tanga 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...