Katibu wa Baraza la Vyama vya Siasa anatumia fursa hii kuwatangazia wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa, tarehe ya kurejesha fomu za wagombe imesogezwa mbele mpaka tarehe 14 Disemba, 2016 saa tisa na nusu (3:30) alasiri, kutokana na siku ya Ijumaa tarehe 09 Disemba, 2016 na Jumatatu tarehe 12 Disemba, 2016 kuwa ni sikukuu.
Fomu zilizojazwa kikamilifu zinapaswa kurejeshwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Dar es salaam.
Sisty L. Nyahoza
Kny: KATIBU WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA
10 Disemba, 2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...