Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) akipokea
vifaa vya michezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SAN LAM Life
Insurance, Bw. Samuel Mika(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa
Jeshi hilo, Kamishna Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) ni Afisa Uhusiano wa
Kampuni ya SAN LAM, Bw. Rishia Kileo. Vifaa hivyo vitatumiwa na Maafisa na
Askari wa Jeshi la Magereza katika Mashindano ya Kijeshi yanayotarajiwa
kufanyika Zanzibar mwezi huu Desemba, 2016.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akitoa neno la shukrani
kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na Kampuni
ya SAN LAM Life Insurance. Hafla hiyo imefanyika leo Desemba 06, 2016 katika
Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Kamishna wa Magereza Gaston
Sanga(kulia) ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni SAN LAM Life Insurance, Bw.
Samuel Mika.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SAN LAM Life Insurance, Bw. Samuel Mika akitoa
maelezo mafupi kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Jeshi la Magereza leo
Desemba 06, 2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar
es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Jeshi la
Magereza, SACP. Gideon Nkana akitoa utambulisho mfupi katika hafla ya kukabidhi
vifaa vya michezo kwa Jeshi la Magereza leo Desemba 06, 2016 katika Ukumbi wa
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati walioketi)
akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja
na Wawakilikilishi wa Kampuni ya SAN LAM Life Insurance(waliosimama). hafla
hiyo ya makabidhiano ya vifaa vya michezo imefanyika leo Desemba 06, 2016
katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...