Wanajumuia ya wanafunzi waliosoma Tumaini University - Iringa, Songea Boys High School na Lugalo Secondary School wanasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa mwanafunzi mwenzao Marehemu Felix Kapinga (pichani) kilichotokea Usiku wa Tarehe 3/12/2016 katika Hospitali ya Ikonda Mission Mkoa wa Njombe baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Tunachukua fursa hii kutoa pole kwa Mke wa marehemu, Mtoto wa marehemu, Mama mzazi wa marehemu, wafanyakazi wenzake kutoka Njombe community Bank, Ndugu, jamaa, Marafiki na wana familia kiujumla kwa msiba huu walioupata, tunaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo tarehe 06/12/2016 huko huko Njombe katika eneo la kijiji kinachotambulika kwa jina la Ramadhani ambako Mama mzazi wa marehemu ndiko anakoishi, shighuli za Mazishi zinategemewa kufanyika kuanzia saa 6.00 Mchana. Kwa taarifa zaidi unaweza ukawasiliana kwa namba
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA
JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMIN.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...