Hatimaye Makampuni matano yanayomilikiwa na Mfanyabiashara Yusuf
Mehboub Manji yameondolewa katika Jengo la Quality Plaza linalomilikiwa na
Shirika la Hifadhi ya Jamii la PSPF. Jengo hilo lipo Kitalu Na. 189/2 na liko
mkabala na Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.
Sababu inayotajwa ya Makampuni hayo kuondolewa katika jengo hilo
ni deni la kodi ya pango linalofikia kiasi cha Shilingi bilioni 13. Hatua
ya kung'olewa makampuni hayo katika jengo hilo ni baada ya mpangaji kushindwa kuondoka kwa hiari
baada ya kupewa notisi ya masaa 24.
Makampuni yaliyoondolewa ni Quality Group Company
Limited, Gaming Management Limited, Q-Consult Limited, Quality Logistics
Company Limited, na International Transit Investment Limited. Jeshi la Polisi lilisimamia wakati kampuni ya udalali ya Yono
Auction Mart ikizihamisha kampuni hizo.
Inadaiwa kuwa Mfuko wa PSPF kwa muda mrefu umekuwa unaidai Kampuni
ya Quality Group fedha hizo za upangaji, lakini kila inapotakiwa kulipa imekuwa
ikikwepa na kukimbilia mahakamani kuweka pingamizi la kulipana kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa Novemba 24, mwaka huu umemtaka aondoke
ndani ya masaa 24 na kulipa deni analodaiwa.
Pia mmiliki wa kampuni hizo, japo amekwisha ondolewa katika jengo
hilo amepewa muda wa siku 14 kisheria awe amelipa deni hilo na kama atashindwa
kulipa mali zake zitakamatwa na kuuzwa ili kupata fedha za kulipa deni
analodaiwa na PSPF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...