Michezo ya saba ya  Mabunge ya Africa Mashariki (7th East African Community Inter- parliamentary games) ilifunguliwa Jana jumapili tarehe 4 Desemba, 2016 kwa michezo ya riadha na kuvuta kamba ambapo Uganda ilionekana kung'ara karibu kwa kila michezo kwa pande zote mbili za wanawake na wanaume.
Michezo hiyo inashirikisha nchi wanachama wa EAC pamoja na Bunge la Jumuiya -EALA ambapo jumla ya Michezo Sita itashindaniwa. Michezo hiyo ni kutembea, riadha, kuvuta kamba, volleyball, netball na soka.Akizungumza wakati wa Ufunguzi Mwenyekiti wa Bunge Sports Club ya Tanzania Mhe William Ngereja alielezea umuhimu wa kuendelea kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia nyanja mbalimbali za kimaisha ikiwa ni pamoja na michezo.

 Wakipeperusha bendera ya Tanzania ni Waheshimiwa Wabunge Ali King, Mussa Sima na Cosato Chumi wakati wa ufunguzi wa michezo hiyo
 Mhe Venance Mwamoto akiongoza katika mashindano ya kutembea kwa haraka wakati wa siku ya kwanza ya mashindano ya mabunge ya Africa Mashariki huko Mombasa
 Wabunge wakimpongeza Mhe Halima Mdee baada ya kufuzu kuingia fainali ya mbio za mita Mia nne za Mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki Jana jumapili kwenye Viwanja vya Mbaraki Sports Club Mombasa
 Wachezaji wa timu ya Bunge Sports wakijiandaa na mchezo wa kuvuta kamba Jana jumapili kwenye Viwanja vya Mbaraki Sports Club huko Mombasa
Wachezaji wanawake wa  timu ya Bunge Sports wakijiandaa na michezo mbalimbali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ulaji wa aina gani hii? Are they serious?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...