Na: Frank Shija – MAELEZO.

 
MAKOMANDOO wa Jeshi la Ulinzi wanatarajiwa kupamba sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo wwatacheza  gwaride  la kimyakimya.
 
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa  leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri Jenista amesema kuwa  mbali na maonyesho hayo pia kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka vikundi vya Bendi ya Muziki wa kizazi kipya na Kizazi cha zamani, ngoma za asili za mikoa ya Mbeya, Pwani, Lindi na kimoja kutoka Zanzibar.

Waziri Mhagama ameongeza kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Aidha ametoa  wito kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Uhuru siku hiyo ya tarehe 9 Desemba ili kusjumuika na Watanzania wote katika kuadhimisha sherehe hizo.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni; “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Kuimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu”  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...