Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii .
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi vifaa mbalimbali kwa wakazi wa Dar es Salaam vyenye thamani ya 164,272,000/= ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika ziara ya Dar mpya.
Makonda amesema kuwa anatimiza ahadi zake kwa wahusika kama ifuatavyo Sober house kigamboni kwa kuwapa jiko la gesi, mitungi 2,king’amuzi televisheni moja ya nchi 49 na magodoro 50 pia ameweza kutoa zawadii ya pikipiki kwa watendaji wa ofsi yake kwa kuwapa morarli ya kazi pamoja na mwenyekiti wa serikali ya mtaa Mivinjeni kata ya buguruni.
Aidha mkuu wa mkoa ametoa zawadi kwa watumishi wane ambao ni Dr.Grace Magembe,mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Mruto kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke,Edward Otieno katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji na Aron Joseph Mkkurugenzi uendeshaji wa DAWASCO.
Pia ametoa mitaji ya biashara kwa wajasiliamali wawili kwa kwa kukabidhi kiasi cha fedha cha shilingi miioni moja kwa kijana mmoja na shilingi laki mbili kwa mwanamke mjasiliamali kwa ajjili ya kuimarrisha biashara yake.
Msaada mwingne alitoa mkuu huyo wa mkoa ni pamoja na mabati 2000 kwa ajili ya sekondari ya Jeshi ya jitegemee na shule ya msingi Annex Mbagala mabati 1000 na shule ya msingi ya katoliki kupewasaruji mifuko 1000 .
Pia ameimarisha kikosi cha jeshi la wananchi wa Tanzania kwa kutoa Zawadi ya Tumba kwa ajili ya bendi ya jeshi na kutoa zawadi ya gari kwa ajilli ya kuimarisha huduma katika Zahanati ya kikosi cha kikosi cha kutuliza ghasia kanda maalum ya Dar es Salaam Ukonga.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa wakazi wa Dar es Salaam vyenye thamani ya 164,272,000/=leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia kanda maalum ya Dar es Salaam, Acp.Stanley Kulyamo akipokea gari la wagonjwa kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda , akikabidhi shilingi laki mbili kwa mjasiliamali ,Zuhura Waziri mkazi wa Mwembe Yanga kwa ajili ya kuongeza mtaji wake wa Supu.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikabidhi hundi kwa mchungaji Epafra Zabron Shinji wa kanisa la AIC Tanzania.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akikabidhi mifuko ya Saruji kwa Mkuu wa shule ya St Joseph Goba , Sister Caroline Kokutekana, kama sehemu ya kutimiza ahadi yake wakat wa mahafali ya shule hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...