Desemba
18, 2016
Mke wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli leo Jumapili ameungana na
Wakristo wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro iliyopo
Oysterbay Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki kadhaa tangu alipougua na kulazwa
hospitali.
Akiwa mwenye afya
njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wamesali ibada ya asubuhi katika kanisa hilo na baadaye kusalimiana na
waumini nje ya kanisa.
Baada ya
kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wameelezea furaha yao ya
kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na wamemuombea afya njema.
"Nimejisikia
furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya njema na uso
wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee kumsimamia"
amesema Mama Mabula.
"Nimeshukuru
sana kumuona Mama yangu Mama Magufuli, Mwanajumuiya mwenzangu leo Kanisani,
huku afya yake ikiwa imetengemaa zaidi, tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu na
tunamuombea aendelee kumpigania afya yake izidi kuwa imara"
amesema Thomas Simon.
"Kwa
kweli siku ya leo kwangu mimi ninafuraha sana kwa kumuona Mama akiwa kanisani,
na zaidi Mama wote wawili kwa sababu pia amekuja Mke wa Mhe. Waziri Mkuu, kwa
hiyo kwetu sisi ni furaha sana kama Parokia, tunafurahi sana tunaposhirikiana
na viongozi wetu" ameongeza Epifania Ngonyani.
Mwezi uliopita
Mama Janeth Magufuli aliugua na kulazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipata matibabu kwa siku mbili na kisha
kuruhusiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...