Tuna furaha kubwa ya kuwaalika Watanzania
wote wakazi wa mji wa Leicester UINGEREZA na vitongoji vyake kuhudhuria Mkutano
wa Uzinduzi wa Jumuia ya Watanzania Leicester.
Lengo la Mkutano huo ni kuzindua Jumuia
yetu, ambapo Masuala kadha yatajadiliwa, yakiwemo:
Taratibu za kujiunga, Umuhimu wa kuwa na Jumuia
inayotambuliwa na Ubalozi pamoja na Serikali ya Tanzania, Faida Za Kujiunga pamoja na thamani ya Diaspora kwa nchi ya
Tanzania.
Ushawishi
wa kuunda Jumuia hii uliongezwa nguvu na Maofisa Ubalozi wa Tanzania UK mwaka
jana: Walihimiza Haja
ya Watanzania kujikusanya rasmi, lakini pia nia ya Serikali kushirikiana na Diaspora
kujenga Tanzania ya sasa.
Ndugu
zangu: UMOJA NI NGUVU!!
Katika
kipindi hiki Mwaka Mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu,
Wana
Diaspora tuna maswali magumu yanayohitaji kujibiwa haraka!!!!
Tujikusanye,
Tuwasilishe Changamoto zetu ili Tusikilizwe!!!
Jumuia
ya watanzania Leicester itakuwa kiungo muhimu kati ya
Diaspora,
Ubalozi na Serikali.
SIKU: JUMAMOSI 17 DISEMBA 2016
MUDA:
SAA SABA KAMILI MCHANA MPAKA SAA
KUMI JIONI (1.00PM-4.00PM)
UKUMBI:
ST MATTHEWS CENTRE, 10 Malabar Road, Leicester, LE1 2PD
Tafadhali
usikose Kuhudhuria
Tafadhali
nawe tusaidie kualika wengine uwajuao. Shukrani sana!
Kwa Maelezo Zaidi wasiliana na MOSES KUSAMBA Simu: 07903
621150
Pia waweza kuwasiliana na Uongozi wa muda
kwa E mail: tzumojaleicester@gmail.com
KARIBUNI
NYOTE
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...