Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel ameseama sekta ya viwanda inahitaji rasimali watu hivyo kama wadau wanawajibu wa kuandaa rasilimali ya viwanda yenye tija.

Mollel ameyasema hayo leo katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba jijini, Dar es Salaam, amesema GEL inachokifanya kutafuta fursa ya vyuo vya nje ambavyo vinaandaa wataalam katika sekta ya viwanda.

Amesema sekta ya viwanda haiwezi kusonga mbele kama hakuna rasilimali watu wenye ujuzi wa kuendesha viwanda hivyo. Mollel amesema GEL imeshapeleka wanafunzi katika vyuo vya nje ambao wanasomea uhandisi wa viwanda ambapo ndio rasilimali watu tarajiwa katika sekta ya viwanda nchini.

Aidha amesema kama wadau wanawajibu wakuisaidia nchi katika harakati ya sekta ya viwanda ili nchi iweze kupata uchumi huo. ‘’Hatutakuwa sahihi bila kuonyesha mchango katika taifa hili ya kuandaa rasilimali watu ambao wataleta mageuzi ya viwanda’’ amesema Mollel.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage (wakwanza kushoto) akiwa na Naibu Waziri Uchumi na Biashara wa Ukraine, Nataliya Mykolska (wapili kulia) na Naibu Waziri wa Chakula, Olga Trafimstave (wapili kushoto) akitoa maelezo wa ugeni huo walipotembelea banda la Global Education Link (GEL) katika maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel. Katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage akiwa na Manaibu Waziri wa Ukraine, Nataliya Mykolska wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel wakati walipotembelea banda hilo leo katika maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akitoa maelezo kwa wanafuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)walipotembelea banda hilo leo katika maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...