Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limepiga marufuku matumizi ya Mifuko ya Plastiki,katazo litakaloanza kutumika Januari Mosi Mwaka 2017.

Katazo la Matumizi ya Mifuko ya Plastiki limekuja baada ya kubaini kuwa Mifuko hiyo haiozi kwenye udongo.

Akizungumza na Globu ya Jamii,Wakili wa Serikali Mkuu-NEMC,Vincent Haule amesema kuwa Sheria ndogo ya katazo hilo inataka kukataza Mifuko ya Plastiki isipokuwa kwa matumizi ya huduma za matibabu,Vifungashio vya Viwanda,Matumizi ya Ujenzi,Matumizi yakutengeneza Maturubai,Mifuko inayotumika kwenye Kilimo na Usafi.

Pia amesema kuwa Mifuko ya Plastiki itakayosafirishwa Soko la Nje itaruhusiwa,ambayo inaanzishwa Dhamana ya Utumiaji Mifuko ya Plastiki (Plastic Waste Perfomance Bond).

Hata hivyo amebainisha Sheria za kuingia Mifuko ya Plastiki kuwa ni lazima kuwepo kwa Leseni,Lebo maalum.Amesema faini ya kosa la kuingiza Mifuko ya Plastiki ni Milioni 5 ambayo haitazidi Milioni 20,ama kifungu cha miaka 5 ama vyote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...