Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini,Godfrey Simbeye akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya ushiriki wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo(TCCIA), Gotfrid Muganda
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) imesema ni vigumu kwa nchi inayoendelea kama Tanzania kupata maendeleo pasipo kupata mitaji kutoka kwa wawekezaji wa nchi nyingine zenye mitaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu maoni ya TPSF, kuhusu umuhimu wa majadiliano kati ya sekta binafsi na sekta ya Umma katika kuleta mazingira wezeshi ya uwekezaji hapa nchini kwa mwaka 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema mitaji ikipatikana inaweza kuwekezwa katika maeneo mbalimbali na nchi ikaweza kupata maendeleo tunayoyataka hususani katika sekta ya Viwanda.
Amesema serikali aanzishe utaratibu wa kila Wizara kuwa na kitengo kitachokuwa kinaratibu maboresho au mazingira ya biashara katika maeneo kazi yao.
Simbeye amesema serikali imetenga fedha nyingi za maendeleo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 ili ziweze kutumika katika miundombinu ya barabara, reli, uboreshaji wa viwanja vya ndege, uboreshaji wa bandari, miradi ya umeme pamoja Kilimo cha umwagiliaji.
Aidha amesema katika kuyafikia maendeleo hayo kunahitajika kuwepo kwa kamati ya kitaifa ya kusimamia maboresho ya mifumo ya usimamizi wa leseni kwa kuwa na wajumbe wa sekta binafsi na serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...