Skauti kutoka nchi za Afrika ya Mashariki, wapo jijini Arusha kwa mashindano ya stadi za kiskauti ambayo yalianza Jumatatu tarehe 12 Desemba 2016 na yatafikia kilele chake tarehe 16 Desemba 2016.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamishna Msaidizi (Mawasiliano na Habari) wa Chama cha Skauri Tanzania, Bw. Hidan Ricco, Mashindano hayo yanafanyika katika uwanja wa shule ya Breburn International iliyopo eneo la Kisongo Arusha.
Bw. Ricco amesema kwamba sambamba na hayo mashindano Skauti pia wanashiriki katika Jukwaa la Vijana (youth Forum) katika hoteli ya Crown iliyopo katikati ya Jiji la Arusha. sambamba na Mkutano wa Makamishna Wakuu wa Skauti kwa nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Amesema shughuli zote hizo tatu zitafikia kilele chake siku ya Ijumaa tarehe 16 Desemba 2016 na zinatarajiwa kutafungwa rasmi na Mkuu wa Majeshi wa Nchi ya Uganda.
Skauti kutoka Kenya na wengine wa nchi za Afrika Mashariki wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya mashindano ya skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea mkoani Arusha
Kamishna Mkuu wa Skauti Kenya bw. Ray Charles Musau akizungumza na skauti wa nchi za Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa kambi ya mashindano inayoendelea mkoani Arusha.
Skauti wa TZ na wengine wa nchi za Afrika Mashariki wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya mashindano ya skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea mkoani Arusha
![]() |
| Skauti wa Tanzania na wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi rasmi wa kambi ya mashindano inayoendelea mkoani Arusha. |






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...