Katika
gazeti la Mwananchi toleo la Desemba 16 mwaka huu, ukurasa wa 11, kulichapishwa
barua ya Afisa Mifugo mstaafu wilayani Mpwapwa,
Dododma, Bw. Edward Chedego Uledi. Katika barua yake iliyosomeka “Rais Magufuli nisaidie nilipwe stahiki
zangu,” mstaafu huyo alilalamikia kupunjwa mafao yake.
Mtumishi
huyo aliyestaafu tangu 2008, alilalamikia kitendo cha maafisa utumishi kuchelewa kurekebisha taarifa zake kwa
kuzingatia cheo chake cha mwisho na hivyo kusababisha apunjwe mafao na akalipwa
kwa mujibu wa cheo cha zamani.
Serikali
imefuatilia kwa kina na kuona kuna ukweli katika sehemu ya madai ya mstaafu
huyo. Tunapenda kuutaarifu umma kuwa malalamiko ya mwananchi huyo sasa yameshughulikiwa
haraka na Bw. Uledi amejulishwa na kuridhika na hatua zilizochukuliwa.
Akiishukuru Serikali kwa hatua hizo alisema:
“Nimeeleweshwa vizuri, nimeelewa na
naishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kasi hii. Namshukuru sana Rais na
nawapongeza watendaji wote waliojitoa kufuatilia na kutatua malalamiko ya mimi
mwananchi wa kawaida.”
Serikali
inatumia nafasi hii kuvipongeza vyombo vya habari nchini vinavyojitoa na
kujikita katika kusaidia kutatua changamoto za kweli za wananchi. Aidha
tunawakumbusha watendaji wa Serikali kuendelea kufanyakazi kwa bidii, ubunifu,
kasi na kujituma katika kufuatilia na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Imetolewa na:
Dkt. Hassan Abbasi,
Mkurugenzi Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa
Serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...