Mkaazi wa Singida Mjini, Mrisho Joseph mwenye umri wa miaka 23 ameibuka mshindi baada ya kubashiri vyema matokeo ya mechi kupitia Kampuni ya m-Bet na kujishindia zaidi ya Shilingi Milioni 50/-.
Mrisho amekabidhiwa fedha zake leo katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za m-Bet
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa m-Bet, Dhiresh Kabba alisema kuwa Kaungame alifanikiwa kuzoa kitita hich baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi 15 za ligi ya Ulaya kwa mtindo wa kucheza kawaida.
“Tunafarijika kumkabidhi Mrisho Joseph kitita hicho cha Sh milioni 50/- akiwa ndiye mshindi wa m-Bet ambapo amesema atawekeza katika biashara zake ili aweze kusaidia wakazi mbalimbali wa mji wa singida wanaomzunguka,” alisema Kabba.
Aliwataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Perfect 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote unaondoka na kitita chako mchana kweupe na ndicho Mrisho alichofanya.
Naye Mshindi huyo, Mrisho Joseph amewashauri watanzania wote hasa wakazi wa Singida wenye umri unaoruhusiwa kisheria kujitokeza kubashiri matokeo ya mechi mbalimbali kupitia Kampuni ya m-Bet .
"Nashukuru sana m-Bet kwa kuniwezesha kujikwamua kimaisha, nitatumia fedha hizi kutimiza ndoto yangu ya kununua kiwanja na kuanza ujenzi", alisema Mrisho.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimab (kushoto) akikamkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni
50/- mshindi wa M-bet, Mkazi wa Mkoa wa Singida,Mrisho Joseph(kulia)kwenye
hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo,Katikati
ni Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Abbas
Tarimba(kushoto)na Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba,wakimpongeza kwa kumpigia
makofi mshindi wa M-bet, Mkazi wa Mkoa wa Singida,Mrisho Joseph(kulia)wakati wa
hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es
Salaam ya kumkabidhi hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 50/-
mshindi huyo leo.
Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba(kushoto)na
mshindi wa M-bet, Mkazi wa Mkoa wa Singida,Mrisho Joseph(kulia) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Abbas
Tarimba,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi hundi yenye thamani
ya zaidi ya shilingi Milioni 50/- mshindi huyo jijini Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...