
Miaka 25 ijayo,
Takribani asilimia 75 ya wakazi wa Afrika Mashariki watakuwa vijana,na hii
inamaanisha nguvukazi kubwa itakuwa mikononi mwao.
Lakini kama watasalia kuwa
idadi kubwa basi na kuwa na maarifa ya kuendesha nchi, basi changamoto itakuwa
kwa ukuaji wa nchi.Vijana wao huona kama wana mchango katika jamii, hasa kwenye
makusanyiko ya kijamii
mathalani misiba, ambapo hutakiwa kuchangamkia kwenye shughuli zenye uhitaji wa
nguvu.
Lakini kama fursa ya uwepo wa vijana katika jamii itatumiwa vema, basi
nyanja zote za maendeleo zitaendeshwa vema, na watakuwa na uwezo wa kutatuza matatizo
yaliyo kwenye jamii – sawasawa na malengo endelevu namba 2 na namba 8 za umoja
wa mataifa, zinazolenga kumaliza masuala ya njaa, na pia uhakika wa kazi na
ukuaji wa uchumi, ikiwemo pia lengo namba 4 – kuwa na elimu bora.
Uwepo wa Tamasha
la Sifa za Yeriko ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa Maono Foundation
Limited na washirika wake kuwa sehemu ya kutatua matatizo haya kwa kuanzisha
kituo cha ukuzaji wa vipaji kwa vijana, kusudi waweze kuwa sehemu ya suluhu ya
changamoto kwenye jamii.
Mkakati wa muda mfupi, ni kuhudumia moja ya kituo cha
watoto yatima cha Guardian Angels House of Hope chenye uhitaji wa taaluma za
watoto kukuzwa,lakini changamoto ikawa kukosekana kwa ada na mahitaji mengine
ya shuleni.Kwa kujumuika kwenye tamasha hili, si tu kwamba watakuwa
wanamuaibisha mwovu shetani kwa kuangusha ngome zinazowasumbua kwenye Nyanja mbalimbali
maishani, bali pia watakuwa wamechangia katika kutimia kwa malengo ya Maono
Foundation.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...