Na Pascal Mayalla
Tanzania imeanza kutumia vizuri Mabilioni ya Taasisi ya TradeMark East Africa, kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kwa kugharimia mafunzo ya kuwajengea uwezo Wafanyabiashara Wanawake wa Tanzania, walio chini ya mwamvuli wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania , (Tanzania Women Chamber of Commerce, TWCC), ili kuweza kuvuka mipaka na kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na hata nje ya bara la Afrika.
Akizungumzia kuanza kwa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa TradeMark Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, aliyewakilishwa na Program Manager wa TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bi Monica Hangi, amesema, mafunzo hayo ni sehemu ya utakelezaji wa mradi mkubwa wa Taasisi ya Trademark East Africa ujulikanao kama “Women in Trade” unaolenga kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na masoko ya kimataifa.
Taasisi ya TradeMark imetenga Dola za Marekani Milioni 5,300,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 12 za Kitanzania kugharimia mpango huo.
Bi Hangi amesema, “Ukimuwezesha mwanamke, ni kuiwezesha familia nzima, familia zikiwezeshwa ni kuwezesha jamii nzima na jamii zikiwezeshwa na kuwezesha taifa kwa ujumla, hivyo uwezeshaji huo kwa wanawake ni uwezeshaji kwa taifa kupata maendeleo”
Program Manager wa TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania,
Bi Monica Hangi, akitunuku cheti cha kuhitimu mafunzo ya kuvuka mipaka, kwa
mjasiliamali wa Mavazi, Bi. Daria Gwao Makaramba kwenye hafla fupi ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wa
kuvuka mipaka kwa wafanyabiashara wanawake
wa Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake
Tanzania (TWCC) ili kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya Afrika
Mashariki . Mafunzo hayo, yameendeshwa taasisi ya mafunzo ya CABO Consult na
kufadhiliwa na TradeMark East Africa.
Program Manager wa TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania,
Bi Monica Hangi, akitunuku cheti cha kuhitimu mafunzo ya kuvuka mipaka, kwa
mjasiliamali wa kusindika vyakula, Mwal. Rose Romanus kwenye hafla fupi ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wa
kuvuka mipaka kwa wafanyabiashara wanawake
wa Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake
Tanzania (TWCC) ili kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya Afrika
Mashariki . Mafunzo hayo, yameendeshwa taasisi ya mafunzo ya CABO Consult na kufadhiliwa
na TradeMark East Africa.
Program Manager wa TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania,
Bi Monica Hangi, akitunuku cheti cha kuhitimu mafunzo ya kuvuka mipaka, kwa
mjasiliamali kijana, Hadija Ahmed, kwenye hafla fupi ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wa
kuvuka mipaka kwa wafanyabiashara wanawake
wa Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake
Tanzania (TWCC) ili kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya Afrika
Mashariki . Mafunzo hayo, yameendeshwa taasisi ya mafunzo ya CABO Consult na
kufadhiliwa na TradeMark East Africa.
Washiriki
wa mafunzo ya kuvuka mipaka, kwenye hafla fupi
ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuvuka mipaka kwa
wafanyabiashara wanawake wa Tanzania
yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) ili
kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya Afrika Mashariki . Mafunzo
hayo, yameendeshwa taasisi ya mafunzo ya CABO Consult na kufadhiliwa na
TradeMark East Africa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...