Na Adili Mhina, Pwani.

Tume ya Mipango imetembelea kiwanda cha vinywaji cha Azam kilichoko eneo la Mwandege Mkoani Pwani na kuonesha kuridhishwa na shughuli za uzalishaji za kiwanda hicho ikiwa ni moja ya mikakati ya kutekeleza malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Timu ya wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ilifanya mazungumzo na Meneja anayesimamia ubora wa bidhaa kiwandani hapo, Bibi Lilian Mwashigadi na kuelezwa kuwa kiwanda hicho kipo katika hali nzuri na kinaendelea na shughuli za kuzalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa katika kukidhi mahitaji ya soko. 

Bibi Mwashigadi alieleza kuwa kiwanda hicho ambacho kina jumla ya wafanyakazi 800 ambapo kati hao 500 ni ajira za moja kwa moja (direct labor) na 300 ni ajira zisizo za moja kwa moja (indirect labor) kina mikakati ya kuendelea kupanua soko la bidhaa zake kimataifa ambapo kwa sasa kinauza bidhaa katika nchi za Kenya na Rwanda. 

Kuhusu upatikanaji wa matunda ya kutosheleza kiwanda hicho, Meneja huyo alieleza kuwa hakuna changamoto kwani hapa nchini kuna matunda yenye ubora unaokidhi mahitaji ya viwanda na kiwanda chake kinategemea malighafi hiyo kutoka kwa wakulima wadogo wadogo kutoka maeneo mbalimbali nchini.
 Wataalam kutoka Tume ya Mipango wakimsikiliza Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi wakati wa ziara ya Tume ya Mipango katika kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
 Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Lilian Mwashigadi (aliyevaa koti jeupe) akiwaonesha maofisa wa ukaguzi wa miradi kutoka Tume ya Mipango hatua za mwisho za uzalishaji wa juisi katika kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
 Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi (mwenye koti jeupe) akionesha mtambo unaotumika katika uzalishaji katika kiwanda hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...