KAMPUNI ya kuzalisha umeme wa upepo Afrika Mashariki imesema iko kwenye mchakato wa kuingiza umeme huo kwenye gridi ya taifa, baada ya kukidhi vigezo vya kitaifa.

Akizungumza leo Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Rashid Shamte alisema mradi huo unafanywa kwa ushirikiano na taasisi ya fedha ya Kimataifa iliyochini ya benki ya dunia.

Alisema taasisi hiyo imetoa dola za kimarekani milioni 300 kwa ajili ya kufanikisha mradi huo mkubwa, utakaonufaisha sio tu watanzania bali nchi nyingine.“Tutakuwa na miradi mikubwa lakini sasa tunaelekea kuingiza upepo wa umeme kwenye gridi ya taifa, ili tuanze kusambaza nchi nzima, watu watanufaika kwa njia ya upepo,”alisema.

Kampuni hiyo inatarajiwa kuwa na Kongamano la nishati mbadala litakalofahamika kama ‘Off the Grid’ kwa ajili ya kuzungumzia namna ya kuendeleza miradi mikubwa kwa kutumia nishati mbadala.

Alisema dhamira yao ni kuhakikisha wanakuwa na miradi mikubwa itakayofanya kazi katika nchi zilizokusini mwa jangwa la Sahara.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Rashid Shamte akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuingiza umeme wa upepe kwenye grid ya taifa mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa wadau mbalimbali wa umeme.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...