Na Rhoda Ezekiel -
Globu ya Jamii Kigoma,
JUMLA ya miche 200,000 ya miti imetolewa na Shirika la Kuwahudumia wakimbizi UNHCR Wilayani Kakonko, itakayo fidia uharibifu wa mazingira uliofanywa na Wakimbizi waliopo katika kambi ya mtendeli kutokana na ukataji wa miti hovyo kwa ajili ya kujipatia kuni na miti ya kujengea nyumba za makazi ya kudumu.
Akizungumza na mwandishi Globu hii,Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala alisema ujio wa wakimbizi wilayani humo umesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira katika maendeo yanayo izunguka kambi hali inayo weza kupelekea mabadiliko ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mvua katika Wilaya hiyo.
Ndagala alisema baada ya kuona tatizo hilo alizungumza na Uongozi wa UNHCR ambao waliahidi kulitatua tatizo hilo,ambapo kwa kwasasa wameanza kwa kutoa miche laki mbili ambayo itagawiwa katika vijiji vinavyo izunguka kambi hiyo ili kufidia uharibifu ulio fanyika na kuweza kuweka mazingira vizuri  kuepukana na ukame unaoweza kujitokeza baada ya miti kukosekana.
Alisema wakimbizi wamekuwa na tabia ya kuingia vijijini na kukata miti kuichuna ili ikauke kwa ajili ya kuchukua kuni na miti ya kujengea nyumba za kudumu, hali ambayo imepelekea maeneo hayo kubaki bila kuwa na miti.
Aidha Ndagala aliwaomba watumishi wanao wasimamia wakimbizi kuwapatia miche na wao waweze kupanda miti katika kambi hiyo ili kupata mazingira safi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa sasa maeneo mengi hayana mvua kutokana na maeneo hayo kukosa uangalizi na wananchi wengi kukata miti hovyo.
Pia mkuu huyo ameliomba shirika linalo hudumia wakimbizi kutoa njia mbadala kwa wakimbizi kwa kuwapa majiko ya gesi au majiko banifu yanayoweza kupunguza utumiaji wa kuni unaopelekea uharibifu wa miti kwa kutumia kuni nyingi katika kupikia.
"Kambi hii ya mtendeli inawakimbizi zaidi ya elfu hamsini endapo wote watategemea kuni kutoka kwa wananchi wetu hali hii inaweza kupelekea uharibofu mkubwa,wengine wamekuwa na tabia ya kuuchuna mti kwenye ngozi na kuupaka chumvi baada ya muda unakauka iliwaweze kuukata kiurahisi endapo watapatiwa njiambadala ya nishati ya kupikia itasaidia kupunguza uharibifu huo",alisema ndagala.
Kwa upande wake Mkuu wa kambi ya mtendeli Inocent Mwaka alisema shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR imeandaa utaratibu wa kutoa majiko banifu yanayo tumia kuni chache wakati wa kupikia ilikuweza kuzuia uharibifu huo na kuweza kuacha mazingira yakiwa salama.
Alisema katika kufidia uharibifu huo kuna miche mingi ina inaoteshwa katika kambi na kugawa kwa Wananchi wanao ishi jirani na kambi na kuiotesha ilikuweza kuepukana na madhara ya uchafuzi wa hali ya hewa na mabadiliko ya hali ya tabia ya Nchi
 Sehemu ye makazi wa Wikimbizi wilayani Kakonko
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akionyesha jinsi Wakimbizi wanavyo chuna miti na kuipaka chumvi ili ikauke,hali inayopelekea uharibifu wa Mazingira

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...