Katika picha ni baadhi ya polisi wa kutuliza ghasia wakiwa wamewakamata baadhi ya madereva wa bajaji waliokuwa wakifanya fujo kwenye maeneo mbalimbali hasa eneo la Kabwe kwa kuweka mawe barabarani kutokana na mgomo wa kutoendesha shughuli zao mpaka wenzao waliokamatwa na kutuhumiwa na makosa tofautitofa uti ikiwemo, kutokuwa na Leseni ya udereva, Leseni ya bishara pamoja na kupita njia walizokatazwa na mamlaka.
Polisi wakiendelea kuwakamata waliokuwa wakifanya fujo katika eneo la Kabwe jijini Mbeya leo  jioni ambapo jeshi la polisi kitengo cha kutuliza ghasia kilisambaratisha madereva wote waliokuwa wameweka mawe kwenye baadhi ya barabara na kupiga mabomu ya machozi hali iliyopelekea jiji la mbeya kuwa katika tahruki kwa masaa kadhaa.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Baadhi ya wasafiri wakiwa katika moja kati ya usafiri ulioibuka kufuatia mgomo huo wa bajaji na matokeo yake kuwanufaisha madereva wa magari binafsi na bodaboda kusafirisha abiria.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO WA MMG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...