Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Morogoro
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Stevene Kebwe, amesema watu 13 akiweno aliyehusika kumchoma mkuki mkulima mmoja katika eneo la Mikumi, wamekamatwa na kutiwa mbaroni.
Kebwe amesema hayo ailipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambao wapo mjini hapa kwa jili ya mafunzo ya siku moja kuhusu masuala ya utoaji wa hati za kimila katika Wilaya tatu za mkoa huo.
“Serikali imekamata watu 13 mmoja wao akiwa ndiye aliyehusika kumchoma mkuki mkulima huyo huku wengine wakiwa ni wale waliokuwa wakishabikia kitendo hicho. Hivi sasa watu hao wapo katika kituo cha polisi na wanasubiri kufunguliwa mashitaka kwa ajili ya kufikishwa mahakamani”amesema Kebwe.
Aidha, Kebwe alimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwa kusimamia vema upimaji wa ardhi katika mkoa wa Morogoro.Alisema upimaji huo wa ardhi ndio mwarobaini wa migogoro ya ardhi.
Amesema ni vyema serikali na wadau kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji ili wananchi waweze kutambua mipaka ya maeneo yao hatua itakayosaidia kuepusha migogoro ya ardhi hususani baina ya wafugaji na wakulima.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Stevene Kebwe akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya masula ya ardhi wakimsikiliza mkuu huyo wa mkoa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...