Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), leo
wametoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Mkurugenzi wa Uuguzi katika
hospitali hiyo, Bi. Agnes Mtawa amewashukuru wauguzi hao kwa kuonyesha
ushirikiano katika kazi na kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa.
Mtawa aliwaasa wauguzi kuendelea na upendo huo waliouonyesha katika
kipindi chote cha mwaka 2016 kwa kuwa ndio upendo ambao Mungu anataka
wauonyeshe kwa wagonjwa.
Pia, aliwapongeza kwa kukabiliana na changamoto mbalimbali
katika mwaka huu na kuwataka kutumia changamoto hizo kama sehemu ya mikakati ya
mwaka 2017.
Naye Meneja wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja
aliwashukuru wauguzi kwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa katika kipindi chote
cha mwaka 2016. Hafla hiyo imeudhuriwa na zaidi ya wauguzi 70.
Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa akizungumza na wauguzi baada ya wauguzi hao kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo. Zawadi hizo zimepokelewa na mtoto Neema Selemani kwa niaba ya wagonjwa wengine. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Jengo la watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja na Katibu wa Tughe Tawi La Muhimbili, Bw. Faustine Fidelis.
Mkuu wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja akimkabidhi Mkurugenzi wa Uuguzi katika hospitali hiyo, Bi. Agnes Mtawa zawadi maalamu.
Bi. Anna Mponeja akimlisha keki mtoto Neema Seleman Leo katika hospitali hiyo.
Ni wakati wa kufungua Champainge..Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...