Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii

WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dkt. Philip Mpango anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kodi yanayotarajiwa kufanyika Desemba 17,2016 katika Ukumbi wa Mwl.J.K Nyerere Convection Centre Jijini Dar es Salaam.

Katika Mahafali hayo jumla ya wahitimu 558 watatunukiwa vyeti,shahada na stashahada ambapo kati yao wahitimu wa kike ni 201 na wa kiume 357.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Chuo hicho,Prof.Isaya Jairo amesema kwa mara ya kwanza tangu kuzinduliwa kwa mitaala ya Astashahada ya Uzamili na Stashahada ya Uzamili katika Uongozi wa Forodha ya Afrika Mashariki,chuo kitatunuku Astashahada ya Uzamili ya Uongozi wa Forodha ya Afrika Mashariki (Post Graduate Certificate in Customs Administration (PGCCA).

Prof.Jairo amesema Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika Mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutunuku Cheti hiko.Amesema Jumla ya Wahitimu 77 watatunukiwa PGCCA wote kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pia amesema kuwa Chuo kinashirikiana na Mamlaka za Mapato za nchi wanachama wa Afrika Mashariki pamoja na zile za Ukanda wa Maendeleo wa Nchi as Kusini mwa Afrika (SADC) kama vile Botswana,Swaziland,Namibia,
Zambia,Afrika Kusini,Zimbambwe na Malawi katika kuwajengea uwezo Wafanyakazi wa Taasisi hizo.
Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA)akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana maandalizi ya Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kodi,Kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo,Mipango,Fedha na Utawala,Charles Sabuni Kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo,Taaluma,Utafiti na Ushauri,Dkt.Lewis Ishemoi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...