Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akizungumza wakati wa makabidhiano rasmi ya ofisi na Katibu Mwenezi Mstaafu wa CCM, Nape Nnauye (kulia), leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Polepole amemsifu Nape kwamba aliongoza Idara hiyo vizuri na kwa hiyo anaendelea kuhitaji ushauri wake katika kazi zake.

Pia Ndugu Polepole ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, kabla ya kuteuliwa na CCM, juzi, kushika wadhifa wake mpya amesema, atafanya kazi kwa weledi mkubwa huku akiahidi kushirikiana kwa karibu na waandishi wa habari.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akizungumza wakati wa makabidhiano rasmi na Katibu Mwenezi Mstaafu wa CCM, Nape Nnauye (kulia), leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akimsikiliza kwa makini, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi mstaafu, Nape Nnauye alipokuwa akizungumza wakati wa makabidhiano rasmi leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akiagana na Katibu Mwenezi Mstaafu wa CCM, Nape Nnauye (kulia), leo nje ya jengo la Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.Picha na Michuzi Jr.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...