Na.Vero Ignatus Arusha.

Mabalozi wa usalama wa usalama barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani wamefanya zowezi la kutoa elimu kwa abiria pamoja na madereva huku jeshi la polisi wakiwapima madereva ulevi na kukagua ubora wa magari hayo kabla ya kuanza safari kuelekea mikoani

Zowezi hilo limeongozwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani SSP Nuru Suleiman na katika stendi kuu ya mabasi yaendendayo mikoani na nchini jirani Jijini Arusha huku zowezi hilo likiwa na lengo la kuelimisha,kukemea na kuripoti mwenendo mzima unaokiuka sheria za usalama barabarani.

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Suleiman amesema kuwa kampeni hiyo inamafanikio makubwa tangia ianze kwenye wiki ya nenda kwa usalama kwani tangia mwanzoni mwa mwaka 2016 hakuna ajali ya basi iliyotokea na kuleta madhara kwa jamii kwa ujumla.

"Kwakweli tunamshukuru sana Mungu kwani tangia mwaka huu uanze hatujapata ajali ya basi inaonyesha madereva wamepata elimu na wanaitendea kazi na tunawaomba waendelee kuwa makini ili ajali ikiwezekana zisitokee kabisa "alisisitiza kamanda Nuru.

Aidha amesema kuwa wamekuwa wakiwapima madereva ulevi na madereva ambao wanakiuka sheria za usalama barabarani na pale wanapogundulika na makosa wapo wengine wanalipishwa faini na wengine wanapelekwa mahakamanikufutiwa leseni na kuzuiliwa kuendesha chombo cha moto kabisa.
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SSP Nuru Suleiman akiwa katika kituo cha kikuu cha mabasi yaendayo mkoania na nchi jirani ,mkoani Arusha tayari kwa kutoa elimu kwa abiria na madereva leo 19Desemba 2016.Picha pamoja na habari na Vero Ignatus Blog.

Kamanda wa Usalama barabarani akiwa anatoa maelekezo kwa Mabalozi wa usalama barabarani( RSA)Katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jiarani mkoani Arusha leo 19Desemba2016.Picha na habari na Vero Ignatus Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...