Na Ofisa habari Mufindi
Halmashauri
ya Wilaya ya Mufindi imeendelea kustawi katika sekta ya elimu ambapo tathimini ya matokeo ya darasa la saba ya Halmshauri hiyo yanaonesha kupanda kutoka asilimia 80.39 mwaka
2015 hadi asilimia 84.90% mapema mwaka jana, ikiwa ni sawa na
ongezeko la asilimia 4.51.
Akisoma
taarifa wakati wa kikao cha thathmini ambacho huwakutanisha wakuu wa shule zote
za msingi na maaofisa elimu kata, Ofisa elimu taaluma wa Halmshauri ya Wilaya
ya Mufindi Miriamu Ngala amebainisha kuwa tathimini ya ufaulu huo umejumuisha
shule 143, watahiniwa elfu 05 mianne 38 ambapo wavulana ni elfu 02 miatatu 84
na wasichana ni elfu 03 na 54 huku wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa
kuendelea na elimu ya Sekondari wakiwa ni 4,617 sawa
na asilimia 84.9.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William katika picha ya pamoja na na waalimu wakuu wa shule zilizofanya vizuri na kutunukiwa vyet na Fedha
Mkuu wa wilya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William (kushoto) akitunuku chet na Fedha kwa mmoja kati ya waalimu wakuu ambao shule zao zimefanya vizuri.
Walimu wakuu na maofisa elimu kata wakiimba wimbo wakati wakimlaki mgeni rasmi kwenye ukumbi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...