Na Chalila Kibuda,
Globu ya Jamii
Globu ya Jamii
‘’KABLA hujafa hujaumbika ni maneno ya wahenga kuwa unaweza ukawa mzima lakini mwisho wa siku ukapata ulemavu wa kudumu katika maisha’’.
Haya ni maneno ya Fundi wa Kushona Nguo Asiyeona, Abdallah Nyangalilo alipoambiwa afanyiwe oparesheni ya macho katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mwaka 1989, akaambiwa kuwa hataona isipokuwa maumivu ya kichwa yatakuwa yamepungua.
Akizungumza na Michuzi Blog katika darasa la wanafunzi wasiyeona, Nyangalilo amesema kuwa wakati alipokuwa amefanyiwa oparesheni Daktari wa Macho Raia wa Urusi alimuambia kuwa amfundishe kushona ambayo ndio itakuwa kazi yake, alikataa na baadae kukubali na kuanza kufundishwa.
Amesema Daktari huyo alikuwa ana cherehani yake akiwa nje ya kazi hutumia cherehani kushona nguo na ndio cherehani aliofundishwa Nyangalilo
Nyangalilo amesema 1994 alianza kazi ya kushona kwa kutumia ujuzi wa Daktari wake na fundi kufundisha wasiyeona na kuongeza kuwa maisha yalikuwa magumu na baadhi ya watu walikuwa hawamini kazi ya kushona ya mtu asiyeona.
Amesema katika kufanya kazi hiyo ameweza kuendesha maisha yake,licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na hali aliyokuwa nayo ya kuona.Nyangalilo amesema katika kufanya hivyo anaweza kushona nguo kwa kuchukua kipimo cha kushika kiganja cha mkono na kujua saizi zote na kusababisha kuitwa, Dk. Abdallah Nyangalilo.
Amesema Mkurugenzi wa Tan Trade alianza kumwita Daktari kutokana na kazi hiyo wakafika madaktari wa kutoka Norway, Uganda, Kenya na Tanzania na kushauri Mkurugenzi wa Tantrade kuomba kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumtunuku Udaktari wa Heshima, Abdallah Nyangalilo.
Abdallah amesema kwa sasa anafundisha wasio ona wa Manispaa ya Temeke ikiwa ni wasio ona wote wa Jiji la Dar es Salaam na matarajio yake ni kuona anamiliki huo cha kushona cha wasio Ona .
.Fundi wa Kushona Nguo Asiyeona, Dk. Abdallah Nyangalilo akizungumza na mwandishi wa michuzi Blog hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.
Fundi wa Kushona Nguo Asiyeona, Dk. Abdallah Nyangalilo akimpa Maelezo Diwani wa Viti Maalum wa Manispaa ya Ilala (siyeona) , Nuru Awadhi alipotembelea darasa la Dk. Abdallah Nyangalillo. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Mwanafunzi wa Kushona asiyeona, Seif Mdumbe akimpa maalezo Diwani wa Viti Maalum wa Manispaa ya Ilala asiyeona , Nuru Awadhi alipotembelea darasa la Dk. Abdallah Nyangalillo.
Fundi wa Kushona Nguo asiyeona, Dk. Abdallah Nyangalilo akionesha nguo anazoshona kwa Diwani wa Viti Maalum wa Manispaa ya Ilala asiyeona , Nuru Awadhi alipotembelea darasa la Dk. Abdallah Nyangalillo.
Sehemu ya wasiyeona wakiwa katika mafunzo ya ushonaji nguo. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...