Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Taifa linawategemea Vijana  wakati wowote katika dhana nzima itakayothibitisha kwamba wanasimamia kwa vitendo Mapinduzi katika kuondoa maovu yote yanayolikabili Taifa.
Alisema Serikali zote mbili ile na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na iIe ya Mapinduzi ya Zanzibar zinataka kuona  Vijana wake wanakuwa chem chem ya Maendeleo badala ya kuwa dimbwi la matatizo mitaani.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akiyafunga Matembezi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kuunga mkono maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964  hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akivishwa Skafu na Vijana wa Chipukizi kabla ya kuyafunga matembelezi wa UVCCM yaliyohitimishwa hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.

 Vijana wa UVCCM wapatao 400 wakihitimisha matembezi yao ya kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyopokelewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.
 Balozi Seif akipokea Picha ya Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Aman Karume iliyotumiwa na Vijana hao katika matembezi yao. Wa kwanza kutoka kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tanzania Ndugu Shaka Hamdu Shaka na Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo  Bibi Mboni Muhita.
 alozi Seif akipokea Picha ya Muasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere iliyotumika kwenye matembezi hayo.
 Vijana wa UVCCM wakimkabidhi Bendere ya Zanzibar Balozi Seif waliyoitumia kama kielelezo kwenye matembezi yao ya kuunga mkono sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya  
Sehemu ya Vijana wa UVCCM wapatao 400 wakiimba wimbo wa Taifa bada ya matembezi yao ya kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na OMPR, ZNZ. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...