Shirikisho la Soka Duniani Fifa leo linatarajiwa kupiga kura  kuamua kuhusu mpango wa kupanua Kombe la Dunia liwe linashirikisha mataifa 48. Mpango huo ukiidhinishwa, basi utaanza kutekelezwa Kombe la Dunia la 2026, na utakuwa na faida kwa nchi za Afrika na Asia.
Rais wa shirikisho hilo Gianni Infantino (pichani) ambaye amekuwa akipigia upatu  mpango huo na amekuwa na uungwaji mkono mkubwa, pia anataka michuano hiyo iwe na makundi 16 ya mataifa matatu kila kundi na klabu mbili kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya mtoano na iwapo mpango huo utaidhinishwa, basi itakuwa mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kupanuliwa tangu mwaka 1998.
Kuna mapendekezo matano ambayo baraza kuu la Fifa lenye wanachama 37 litaangazia ikiwemo timu 48 na zikiwa kwenye makundi 16 na timu tatu kila kundi ambapo timu mbili bora zitasonga kwa hatua ya mtoano na kuingia timu 32 (mechi 80 kwa jumla).
Mapendekezo mengine ni kuwa na timu 40 na makundi 10 ya timu nne kila kundi ambapo mshindi, na timu sita pekee zinazomaliza nambari mbili kundini ndizo zinafuzu (mechi 76) nyingine ni kuwa na timu 40 na  makundi manane ya timu tano kila kundi (mechi 88) kusalia na kuendelea kusalia na timu 32 .
Infantino, 46, ambaye alimrithi raia mwenzake Sepp Blatter kama rais wa Fifa mwezi Februari 2016 alifanya kampeni akiahidi kupanua michuano hiyo. Awali alipendekeza michuano ya timu 40, wazo lililowasilishwa na rais wa wakati huo wa Uefa Michel Platini 2013, kabla ya kubadilisha msimamo na kuunga mkono michuano ya timu 48.
Chini ya mpango wa Infantino anaoupendekeza kwa sasa, mechi zinaongezeka kutoka 64 hadi 80, lakini fainali bado zinaweza kuchezwa kwa kipindi sawa na cha sasa cha siku 32. Taifa halitatakiwa kucheza zaidi ya mechi saba, sawa na ilivyo chini ya mpango wa sasa na dhaifu pekee ni kwamba huenda mikwaju ya penalti ikatakiwa kutenganisha klabu zinazotoka sare kwenye makundi.
Historia ya Mabadiliko Kombe la Dunia

Kombe la Dunia Timu
1930 Uruguay 13
1934 Italy 16
1950 Brazil 13
1954 Switzerland 16
1958 Sweden 16
1974 West Germany 16
1982 Spain 24
1986 Mexico 24
1998 France 32

Kwa msaada wa BBC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...