Captain Denis Mshami wa wakala wa ndege za serikali napenda kuwashukuru wote kwa upendo na faraja mlioonesha wakati wa msiba pamoja na arobaini ya mke wangu mpenzi Husna Kiluvia Mshami.

Ni watu wengi sana wa kuwashukuru lakini baadhi ya hawa wachache iwe ni uwakilisho wa wengi waliotufariji pamoja na kumuuguza Husna.
Nao ni madaktari ya Hindu Mandal, Dar Group Hospital, Dr Mvungi, Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi, Wakala wa Ndege za serikali chini ya Capt. Raymond Musingi, Michuzi blog, majirani pamoja na ndugu jamaa na marafiki. Tunapenda kusema tena asante sana.
Husna, leo ni tarehe 7.01.2017 umetimiza miezi miwili toka uondoke. Nilikupenda sana na nitakupenda siku zote. Mwenyezi Mungu akupe pumziko la amani. Amina.
"Wote wamwaminio Mungu watatambua ukweli wake;wote walio waaminifu watakaa upande wake kwa upendo, maana huwajalia neema na huruma watakatifu wake. Na huwaangalia kwa wema hao aliowateua".
(Hekima ya Sulemani 3:9)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...