Mwili wa marehemu mze Boniface Pangawe Lukosi umesafirishwa jana Ijumaa Januari 6, 2017 kuelekea kijijini kwake Kalenga mkoani Iringa baada ya misa na kuagwa katika kanisa la Mtakatifu Yohana lililopo Yombo Vituka jijini Dar es salaam.
Marehemu mzee Lukosi, aliyefariki Januari 3, 2017 akiwa na umri wa miaka 95, anatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi Januari 7, 2017 kwenye makaburi ya familia hapo Kalenga. Ndugu, jamaa, marafiki na majirani walijitokeza kwa wingi kuaga mwili wa marehemu, kabla ya jeneza lake kuingizwa kwenye basi na kuanza safari majira ya saa kumi jioni. Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi - AMINA
Sehemu ya ndugu, jamaa, marafiki na majirani waliojitokeza kwa wingi kwenye misa na kuaga mwili wa marehemu. Aliyebeba mtoto ni mdau Chef Issa wa Sweden ambaye yuko mapumziko mafupi na nyuma yake mwenye fulana ya pundamilia ni mdau Dr. D. Ruhwago
Wafiwa wakiongozwa na mdau Chris Lukosi wakiwa kanisani hapo
Baba Paroko akiombea mwili na wafiwa safari njema
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiingizwa garini tayari kwa safari
Mdau Chris Lukosi katika majonzi
Mdau Chris Lukosi akitambulishwa kwa Chef Issa na mdau Seraphin na Dr. D, Ruhwago ambao ni baadhi ya wadau waliofika kumfariji mwanagrupu mwenzao anayeishi Uingereza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...