Serikali mkoani Njombe imewataka wakulima kujiunga katika vikundi vya ushirika ili waweze kufikiwa kwa urahisi na mradi wa uzalishaji na usambazaji mbegu bora za viazi mviringo unaoratibiwa na Mpango wa kuendeleza kilimo  ukawanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Katibu Tawala Msaidizi (Sekta ya Uchumi na Uzalishaji),Bw.Lameck Noah alisema ni vyema wakulima wakajiunga katika vikundi ili waweze kufikiwa na miradi mbalimbali na hata huduma nyinyine.

“Lazima tukubali kubadilika kifikra na mtazamo tutoke katika kilimo cha mazoea na tufanye kilimo cha biashara” alisema Bw. Noah

Alisisitiza kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi itubadilishe katika kufanya kilimo kinachoendana na upatikanaji wa mvua kuepuka mazao kuharibika kwa kukosa mvua.
 Alisema mradi umelenga kuwainua wakulima kwa kuwapa mbinu mpya za kilimo na mbegu bora zitakazopelekea kupata mavuno mengi tofauti na hali ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

Alisisitiza kuwa wakulima walikuwa wanaacha viazi vingi ardhi kwa sababu ya kutumia jembe la mkono wakati wa kuvuna, sasa mradi huu umekuja na mbinu mpya ya kulima kwa kutumia mashine na hivyo itapelekea mavuno kuongezeka.

“Mradi huu hautawafikia wakulima wengi kama hawatajiunga katika vikundi katika maeneo yao,” alisema Bw.Noah

Alisema SAGCOT inatoa mafunzo na mbegu bure kwa wakulima sasa ni vyema wakawa katika umoja ili waweze kufikiwa kirahisi na mradi na pia kwa wale walikwisha nufaika na mafunzo wajitoe kuwaelekeza na wengine ili tuongeze uzalishaji katika Mkoa.

Alisema mafanikio baada ya mradi kwa baadhi ya wakulima ni mazuri kwani sasa wameweza kuvuna magunia 70 mpaka 90 kwa hekali tofauti 20 mpaka 30 kabla ya mradi kuwafikia.

“jukumu letu serikali na kwa kushirikiana na wadau wengine ni kuhakikisha zao la viazi linakuwa na soko la uhakika ndani na nje ya nchi,” alisema Bw.Noah

Alisisitiza kuwa swala la ufungashaji ni changamoto kubwa kwa wakulima hivyo elimu zaidi yahitajika katika kuongeza thamani ya zao hili ili lipate soko la uhakika.

Kwa upande wake Bw.Andrew Mtega mkulima toka Matunda group, Mhaji, Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe, Mkoani Njombe alisema mafanikio yaliyopakwa wakulima wenzetu wa kata ya Mtwango imetupa hamasa ya kuanzisha kikundi.

“SAGCOT wametupatia mafunzo na mbegu bora za viazi kama kikundi kwa sasa tumeweza kupata shamba ambali tutalitumia kupanda mbegu bora kwa njia za kisasa,” alisema Bw.Mtega
Alisema elimu tuliyopata na mafanikio yatakayopatikana baada ya mavuzo yatakuwa kielelezo tosha cha kuwahamasisha wakulima wengine kupata mafunzo na kutumia mbegu bora za viazi.

SAGCOT inaratibu mradi wa uzalishaji na usambazaji mbegu bora za viazi mviringo katika mkoa wa Njombe kwa lengo la kukuza uzalishaji na kumuongezea kipato mkulima. Mradi huo umefadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekali(USAID) kupitia Shirika la kusimia mapinduzi ya kijani barani Afrika (AGRA) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...