JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) itatoa Ruzuku ya  jumla ya Shilingi Bilioni 7.481 kwa Wachimbaji Madini Wadogo 59 ambapo kiwango cha juu cha Ruzuku kwa Kikundi/Mtu binafsi ni  Shilingi Milioni 210.

Hafla ya utoaji wa Ruzuku hiyo itafanyika siku ya Jumanne,  tarehe 17  Januari 2017, Mjini Mpanda mkoani Katavi, Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim  M. Majaliwa (Mb.).

Fedha za Ruzuku kwa kila Mnufaika, zitatumika kununua vifaa vya kuchimbia au kuchenjulia madini ambapo kabla ya kukabidhiwa vifaa hivyo, wanufaika hao watapata mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya ruzuku yatakayotolewa na Wizara ya Nishati na Madini tarehe 16 Januari, 2017 Mjini Mpanda.

Miradi 59 itakayopata ruzuku hiyo, ndiyo iliyoshinda kati ya miradi 592 ya uchimbaji madini mdogo iliyokuwa kwenye ushindani.. Waombaji wengine ambao maombi yao hayakushinda watajulishwa kwa Barua.

Wizara ya Nishati na Madini ilianza mchujo wa kuwapata Washindi tangu Mwezi Julai 2016, kwa kuwashirikisha Viongozi wa Wachimbaji Madini Wadogo wa mikoani (REMA’s),Viongozi wa Kitaifa  (FEMATA) pamoja na Viongozi wa Wachimbaji Madini Wanawake (TAWOMA).

Majina ya wanufaika wa Ruzuku awamu ya tatu  pia yanapatikana kwenye Tovuti ya Wizara: www.mem.go.tz pamoja na Ofisi Za Madini Za Kanda.
Imetolewa na,

Prof. Justin W. Ntalikwa
KATIBU MKUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...