Dotto Mwaibale, Kisarawe
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani imetenga Kata 10 kwa ajili ya kilimo cha mkataba kitakachoendeshwa na Taasisi ya Winamwanga Cultural Heritage Association.
Mratibu wa mradi huo kutoka taasisi hiyo, Saidi Simkonda akizungumza juzi katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani humo juzi alisema mradi huo umelenga kuwainua kiuchumi wananchi wa Kisarawe na Mkoa wa Pwani kiujumla.
Alisema taasisi hiyo imepanga kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ili kuinua uchumi wa wananchi kupitia vikundi vya ujasiriamali wa kilimo hai na ufugaji wa kuku chotara pamoja na kuwawezesha kupata fursa za mikopo katika asasi za kifedha zilizopo wilayani humo.
"Taasisi yetu imejipanga kuanzisha kilimo cha mkataba ambapo mazao yatakayopatikana itayanunua na tayari serikali ya Kijiji cha Kuluwi imetoa ghala la kuhifadhia mazao hayo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera alisema mradi huo utawasaidia wananchi na kuwa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imetenga kata kadhaa kwa ajili ya mradi huo ambazo ni Maluwi, Vikumburu, Kuluwi na Mafizi.
Alisema kwa sababu mradi huo ni mpya katika wilaya yao na utafanya shughuli zake kwa kilimo cha mkataba aliishauri taasisi hiyo kujenga ushirikiano mkubwa na wananchi kupitia vikundi ambavyo tayari vimesajili na majina yake kuwepo katika daftari ofisini kwa mkurugenzi wa halmshauri hiyo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa kilimo cha mkataba kupitia Taasisi ya Winamwanga Cultural Heritage Association kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera akihutubia wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina ya siku moja iliyohusu kilimo cha mkataba iliyofanyika juzi wilayani humo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa mradi huo, Mwajuma Motto, Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo, Esabela Luoga.
Semina ikiendelea.
Meza kuu.
Mmoja wa maofisa wa Taasisi hiyo, Wilson Kibugu akitoa maelezo kwa wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina hiyo ya siku moja iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...