Habari na Mwene Said wa Blogu ya Jamii, Dar es Salaam.

Koplo Lugano (39),katika kesi ya kuhujumu uchumi dhidi ya raia wa China, Yang Glan maarufu kama Malkia wa pembe za ndovu (66) amedai mahakamani kuwa alishiriki kumkamata mshtakiwa wa tatu Manase Philemon (39).

Koplo Lugano ambaye ni shahidi wa Upande wa Jamhuri, pia ni mpelelezi kutoka Kituo cha Polisi Stakishari, alidai kuwa alifanikisha kumkamata mshtakiwa huyo akiwa katika sehemu ya starehe njiapanda ya majumba sita kwa kushirikiana na makachero wenzake.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alidai kuwa yeye ni mwajiriwa wa jeshi la polisi katika idara ya upelelezi.

Alidai kuwa Aprili 18, 2014, aliitwa na bosi pamoja na wenzake na kupewa jukumu la kumtafuta na kumkamata Manase kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili wa meno ya tembo.“Tulianza msako baada ya kupata taarifa kwamba Manase anapendelea kukaa sehemu mbalimbali za starehe… Aprili 20,2014 tulifanikiwa kumkamata eneo la Njiapanda ya Segerea” alidai.

Akifafanua zaidi shahidi alidai kuwa baada ya kufanikiwa kumkamta walimuweka chini ya ulinzi na kumfikisha kituoni, walipomhoji kuhusu tuhumu hizo alifikishwa mahakamani.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Februari 16 na 17, mwaka huu.

Katika kesi ya msingi,Glan na wenzake wanakabiliwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh. Bilioni 5.4.

Mbali na Glan na Manase, mshtakiwa mwingine ni, Salvius Matembo (39) wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,mwaka 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za serikali ikiwamo meno ya tembo.
Pia, washtakiwa wanadaiwa wakati wa tukio la kwanza walikutwa na wakifanya biashara ya vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 1889 zenye thamani ya Sh bilioni 5.4 bila ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Katika shtaka jingine, ilidaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, mwaka 2014 kwa makusudi Glan akiwa raia wa China, aliongoza na kufadhili kufanyika makosa ya jinai kwa kukusanya na kusafirisha vipande hivyo 706 vya meno ya tembo bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Kwa upande wa washtakiwa Salvius na Manase wanadaiwa kuongoza makosa ya kuhujumu uchumi kwa kusaidia biashara ya nyara za serikali kwa kukusanya, Kusafirisha na Kuuza Meno ya Tembo kwa nia ya kujipatia faida.

Ilidai kuwa Mei 21, mwaka 2014 katika eneo la Sinza Palestina wilaya ya Kinondoni mshtakiwa Manase alitoroka chini ya ulinzi halali wa askari wa Jeshi la Polisi D 7847 Koplo Beatus ambaye alikuwa akimshikilia kwa makosa ya kujihusisha na biashara za nyara za serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...