NA Anthony John Glob jamii

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amelitaka jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kuwakamata wale wote ambao hawajafika kuripoti kituoni hapo kwa tuhuma za uuzaji na uvutaji wa madawa ya kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo Mhe. Makonda amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao walitakiwa kuripoti katika kituo cha kati cha polisi  na hawajafika ambao ni Rashidi makwilo (chidi benzi, Sameer Kheri (mr blue) pamoja na wamiliki wa klabu za kuuza pombe.
"Kuna watu waliowaita lakini mpaka sasa hawajafika. Naliagiza jeshi la polisi kuwakamata na kuwaweka ndani wote ambao hawajafika mpaka juma tatu", amesema.

Sambamba na hayo Mkuu huyo wa mkoa ameongeza majina matatu ya askari polisi na wasanii ambao wanatakiwa wakamatwe kwa tuhuma za kushirikiana na wauza madawa ya kulevya pamoja na Vanesa Mdee na mwana dada Tunda kufika katika kituo cha kati.

Makonda ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kutokomeza hali ya uuzaji na uvutaji wa madawa ya kulevya hapa nchini.
 Mwanadada maarufu hapa jijini Dar,Wema Sepetu akiongozwa na Mmoja wa Makachero wa kituo kikuu  cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam wakiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya
 Mmoja wa wasanii anaetambulika kwa jina la kisanii Babuu wa Kitaa akiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya
 Baadhi ya watu waliofika kituo cha polisi kati kujionea watuhumiwa mbalimbali wa Madawa ya kulevya walioitikia wito wa kuitwa kutoka kwa RC Paul Makonda
  Mmoja wa wasanii mahiri wa bongofleva,maarufu kwa jina la kisani T.I.D akiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Sisi Wa-Tanzania ni watu wa ajabu. Wakati huu, tuna hii dhana ya hapa kazi tu, inayomaanisha kuwa tuko katika kufanya kazi kwa bidii. Papo hapo, yanapotokea matukio mitaani, kunakuwa na mafuriko ya watu wanaojitokeza kushuhudia au kushangaa. Je, huo ndio utekelezaji wa kauli mbiu ya hapa kazi tu?

    Mijadala ya Bunge haionyeshwi papo kwa papo katika televisheni, kwa hoja kwamba itazuia watu kufanya kazi. Je, ni bora zaidi umati wa watu kumwagika mitaani kushuhudia matukio yasiyo na tija au kuangalia mijadala ya Bunge ambayo inaelimisha?

    ReplyDelete
  2. Hili sakata watafutwe na mapapa ambao ndio vyanzo vikuu wakipatikana hao Dar es Salaam itakuwa na neema kubwa mfano nasikitika nikiwa muhimbili hospitali wanapokwenda vijana ambao ni waathirika kwenda kupata dawa yaani inatia imani kubwa Serikali naomba isirudi nyuma watakaobainika kuwa ndio mapapa wafungwe maisha kwa kuwa ni wauaji wa taifa la kesho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...