Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kampuni ya Bima ya UAP na Old Mutual   imetoa mafunzo kwa wadau wa kilimo Tanzania,katika kuwezesha wakulima  kupata bima ya kilimo kwa ajili ya majanga yatakayojitokeza katika kilimo hicho.
Akizungumza katika mafunzo hayo kwa Taasisi za Fedha  yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam,  Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bima hiyo , Raymond Komanga amesema kampuni ya  bima imekuwa ikitoa bima katika kilimo kwa miaka mitatu na kutaka taasisi za fedha kutoa mikopo katika kilimo.
Amesema aina za bima zilotewazo na kampuni hiyo ni  bima za  ukame, mafuriko, Wadudu waharibifu kama nzige, moto, Magonjwa ya Mazao, Upepo mkali pamoja na uharibifu utokanao na mvua za mawe au barafu katika mashamba.
Komanga amesema katika kuendesha bima katika kilimo kampuni imeenda mbali katika kutoa bima ya Mifugo kwa ajili Ukame, Magonjwa ya Mlipuko pamoja na ajali ambayo imaweza kutokana mifugo kufa wakati ikisafirishwa.
Taasisi za fedha  zilizoshiriki mafunzo hayo ni Benki  ya Akiba, NBC and Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania  (TADB) na wadau wengine ambao wanamchango katika sekta ya kilimo ili kuwa ni kilimo chenye tija kwa mkulima.
“UAP Tanzania imekuwa ikitoa bima za kilimo na mifugo kwa miaka mitatu sasa, uwelewa na mwitikio wa bima hizi umekuwa ukiongezeka siku baada ya siku nchini ili kuwafikia wakulima na wafugaji wengi nchini tumeamua kuwahusisha wadau wengine wa kilimo yakiwemo mabenki yanayowakopesha wakulima”amesema Komanga.
 
Aidha amesema mafunzo ya  wadau  wa kilimo itasaidia kupanua wigo wa uelewa na kuwafikia wakulima wengi nchini kwa kuwafanya wakulima na wafugaji kwenda kisasa ya kuwa na  kinga katika  shughuli zao.
 
 Ameongeza kuwa bima ni miongoni mwa vitu vinavyofanya mkulima na mfugaji  kuwa wa kisasa na kuleta ufanisi na mapinduzi ya kilimo nchini.
 Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bima  ya UAP na Old Mutual  , Raymond Komanga akitoa maelezo kwa mdau wa kilimo aliyehudhuria mafunzo ya  wadau wa kilimo juu ya kutumia bima katika kilimo na ufugaji leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa Mafunzo wa Wadau wa Wakilimo watakaowezesha kilimo kuwa na Bima iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja wadau wa kilimo walioshiriki mafunzo juu ya kutumia  bima  ya kilimo na Ufugaji leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...