Vodacom yazindua simu mpya ya Smart Bomba
· Matumizi yake yapo kwenye lugha ya Kiswahili
· Inauzwa ikiwa imeunganishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 30 za buree kwa miezi 3!
Dar es Salaam,Jumatano Februari 03,2017:Sasa ni wakati wa watanzania kufurahia ubunifu wa kiteknolojia wa mawasiliano unaoendana sambamba na mazingira yao halisi na kufurahia kupata taarifa na burudani kwa njia ya interneti ambapo kuanzia leo wateja wa Vodacom,mtandao unaoongoza nchini wataweza kujipatia simu za kisasa zinazotumia interneti aina ya Smart Bomba.
Simu za Smart Bomba ambazo zimezinduliwa rasmi nchini leo zinapatikana kwa gharama nafuu ya shilingi 99,000/-muundo wa matumizi yake uko katika lugha ya taifa ya Kiswahili pia zinanunuliwa zikiwa tayari zimeunganishwa na kifurushi cha interneti chenye GB 10 za buree kwa mwezi na ofa hii inatolewa katika kipindi cha miezi 3 mfululizo kwa ajili ya kumuwezesha mteja kupata na kufurahia intanenti yenye kasi kubwa ya Vodacom mahali popote na wakati wowote.
Mbali na muundo wa matumizi ya simu hii kuwa katika lugha ya Kiswahili na kwendana na mazingira halisi ya maisha ya watanzania walio wengi,simu za Smart Bomba zina umbo la kuvutia,nyepesi na zina kioo cha mbele,cha ukubwa wa kutosha,zinafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya android inaongeza kasi ya kuperuzi internet,inayo kamera ya kurekodi na kupiga picha kwa kiwango chenye ubora wa hali ya juu vilevile inao mfumo wa utambuzi wa ramani ya maeneo mbalimbali ujulikanao kama GPS ambao unatoa maelekezo kuonyesha mahali mtu alipo na mahali aendapo kwa urahisi hususani madereva wa teksi ambao huwapeleka wateja wao sehemu mbalimbali wasiozijua,na zimeunganishwa na program za simu za kurahisisha Maisha za Vodacom kama vile M-Paper.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu hii,Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya Dar es Salaam,Domician Mkama,alisema wakati ni huu wa kila mtanzania kuweza kufurahia matumizi ya simu za kisasa zinazotumia internet (Smart Phones) kwa ajili ya kupata taarifa na burudani kutoka mitandaoni kutokana na kupatikana kwa mara ya kwanza kwa gharama nafuu nchini.
“Kuingia sokoni kwa simu za Smart Bomba za gharama nafuu na zilizotengenezwa kwendana sambamba na mazingira na Maisha ya watanzania walio wengi zikiwa zimeunganishwa na GB 30 kwa matumizi ya miezi 3 ya mwanzoni ni ofa ya kipekee ambayo imebuniwa kubadilisha maisha ya wateja wetu walio wengi na kuendelea kuyafanya kuwa murua”.
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya Dar es Salaam, Domician Mkama(kushoto) akimshuhudia Balozi wa kampuni hiyo,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond Platinumz” akiongea na wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi chenye intanenti ya GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3.
Balozi wa Vodacom Tanzania,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond Platinumz” akiongea na wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya Dar es Salaam, Domician Mkama.
Balozi wa Vodacom Tanzania,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond Platinumz” akiwaburudisha wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...