.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (Mb) kesho Februari 23, 2017 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa miguu kwa vijana na wanawake.
Uzinduzi huo utakaofanyika saa 5.00 asubuhi, utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Mkurugenzi wa Michezo, Yussuph Singo. Utafanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Courtyard, Upanga jijini Dar es Salaam.
Mfuko huo uko chini ya Mwenyekiti Bw. Tido Mhando ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Azam Media wakati Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo ni Bw. Dereck Murusuri.
Wajumbe wake ni Bi. Beatrice Singano, Bw. Ephraim Mafuru, Bw. Tarimba Abbas, Bw. Joseph Kahama, Bw. Salum Rupia na Bw. Meshack Bandawe. Majukumu ya Kamati ya Mfuko huo ni kukusanya rasilimali kwa ajili ya kuendeshea program za TFF za maendeleo ya mpira wa vijana wa wanawake.
vipi watoto wa kuanzia miaka 10 wanawezaje kupata fursa ya kujiunga na kuchukua mafunzo ya mpira wa miguu kwani shule nyingi hawana mpango huo siku hizi inakuwa vigumu kwa wale watoto wenye kupenda kupata msaada wa kukuza vipaji vyao je kuna msaada wowote kwa watoto hAWA?
ReplyDelete