Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akiweka mchanga kwenye jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mafuta na Gesi katika mji wa Kalemie. Kulia kwake ni Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia mbele) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kalemie, Kongo kwa ajili ya kushiriki mkutano wa kubadilishana data na uzoefu kuhusu mafuta katika Tanganyika uliofanyika hivi karibuni nchini Kongo. Nchi nyingine zilizoshiriki ni pamoja na Burundi, Kongo na Zambia. Wengine kutoka kushoto ni Gavana wa Jimbo la Tanganyika – Kongo, Richard Ngoy Kitangala, Waziri wa Migodi na Madini Nchini Zambia, Chris Yaluma na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) na Gavana wa Jimbo la Tanganyika – Kongo, Richard Ngoy Kitangala (kulia) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa (hayupo pichani) katika mkutano huo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria, Wizara ya Nishati na Madini, Anna Ngowi (kushoto) pamoja na wataalam wengine kutoka Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika mkutano huo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...