Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem ameanzisha mradi wa “ MAABARA YA SAYANSI KWA KILA SHULE” ili kusaidia sekta ya elimu nchini ikiwa ni kutikia haraka wito wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli ambaye aliwaomba mabalozi wa nchi za kigeni na wakuu wa mashiriki ya kimataifa na asasi za kiraia kusaidia kwa hali na mali sekta ya elimu na kuzipatia shule vifaa vya elimu kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu katika shule nchini.
Ubalozi wa Kuwait katika ripoti yake kwa vyombo vya habari ulieleza kuwa Balozi Al-Najem amechagua shule moja ya sekondari hapa jijini Dar es salaam kuiandalia maabara itakayokuwa na vifaa vyote vya somo la Kemia na Fizikia kwa gharama za ubalozi, lengo na madhumuni ni kuwaandalia wanafunzi mazingira mazuri ya kusoma masomo ya sayansi kabla ya kujiunga na vyuo vikuu.
Balozi Al-Najem ameeleza kuwa ana matarajio kuwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanyakazi hapa nchini na jumuiya za Kuwait zitaunga mkono mradi huo wa Ubalozi ili ufanikiwe na hatimaye shule nyingine zinufaike.
Kwa upande wake afisa elimu wa Dar es salaam na mjumbe wa baraza la Manispaa ya Kinondoni Bibi Kandiba Ali ambaye alishiriki katika hafla ya kuandaa maabara alisema kuwa mradi huo umekuja katika wakati munasaba ambapo wizara ya elimu itautangaza ili uungwe mkono na pande mbalimbali.
Aidha aliishukuru nchi ya Kuwait, Mfalme, serikali na watu wake kwa kuendelea kuitikia wito na kuunga mkono miswaada ya Tanzania katika sekta mbalimbali hasa elimu na afya.
Yafaa kueleza kuwa ubalozi wa Kuwait uliwahi kuanzisha mradi wa “ KISIMA KWA KILA SHULE” ili kuziba pengo la ukosefu wa maji safi na salama ya kunywa, mradi ambao ulipokewa vyema na maafisa wa serikali ya Tanzania.
Ubalozi wa Kuwait kwa kushirikiana na asasi za misaada za Kuwait umezindua visima vingi katika shule za Dar es salaam na Tanga, pia Asasi ya mwezi mwandamo Red Crescent ya Kuwait hivi karibuni ilisaini mkataba na asasi ya African Relief ya Tanzania kwa ajili ya kuchimba visima 16 katika shule tofauti ili kuwapatia maji ya kunywa maelfu ya wanafunzi, na hivi sasa wasamaria wema kutoka Kuwait wako mbioni kuzindua visima vingine nchini.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akiwa katika shule ya Cordoba Girls Secondary school iliyoko Mikocheni jijini Dar es salaam ambayo ni mojawapo ya shule zilizonufaika na mradi alioanzisha wa “ MAABARA YA SAYANSI KWA KILA SHULE” ili kusaidia sekta ya elimu nchini
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akikagua maabara katika shule ya Cordoba Girls Secondary school
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akiwa na wanafunzi wa shule shule ya Cordoba Girls Secondary school baada ya kukagua maabara yao
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akikagua sehemu ya maabara alizochangia shule ya Cordoba Girls Secondary school
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem katika picha na wanafunzi na walimu wa shule ya Cordoba Girls Secondary school
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...