Na Fredy Mgunda,Iringa.
MASHINDANO ya kombe Mbuzi Cup
yatafikia tamati tarehe 30 mwezi wa tatu kwa kuzikutanisha timu za Mkwawa Rangers
na Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na fainal hiyo itachezwa katika kijiji
cha Kalenga kata ya Kalenga wilayani Iringa mkoani Iringa ikiwa lengo la kuinua
vipaji wa wachezaji kata hiyo.
Akishudia mchezo wa nusu
fainal kati ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) na
timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga katibu tawala
wilaya
ya Iringa Joseph Chitinka ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema ni wakati mzuri
kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia
kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo
yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,
"Mashindano haya ni
muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na
kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo
hiyo" alisema Chitinka
Aidha Chitinka aliongeza kwa
kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza
kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa
vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwasalimia wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya kijiji cha Mangalali kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...