Na Rhoda Ezekiel Kigoma
KATIKA kuelekea siku ya Wanawake Duniani, Baafha ya Wanawake Mkoani Kigoma Wamewaomba Wanaume Mkoani humo kuacha tabia ya kuwanyanyasa wanawake kwa kuwaachia majukumu ya kuzihudumia familia zao, hali inayosababisha Watoto wengi kukosa elimu na wanawake kushindwa kufikia Malengo yao ya kujikomboa na umasikini.
Akizungumza na Globu ya Jamii ofisini kwake jana, katibu wa umoja wa Wanawake Mkoani Kigoma , Salome Luhinguranya alisema kumekuwa na tabia ya Wanaume wengi kukimbia familia zao na kuwaachia mzigo wa malezi na kusomesha watoto wanawake wao hali inayo wapelekea wanawake wengi kishindwa kufanikiwa katika biashara zao kuyokana na Mzigo mkubwa unao Walemea.
Luhinguranya alisema Watoto wengi wamekuwa wakikosa elimu Mkoani humo kutokana na matatizo ya Wanajme wengi kuwatelekeza wake zao na familia zao na kwenda kuoa wake wengine hali inayo wapelekea Wanawake kushindwa kuhudumia familia zao kutokana na ufinyo wa mitaji waliyo nayo.
"Kauli mbiu ya Mwaka huu katika maadhimisho ni Tanzania ya Viwanda wanawake ni msingi wa mabadiliko Kiuchumi,kuelekea. Mkoa wa kigoma wanawake wengi wanajishughulisha katika Shughuli mbali mbali na Wengine ni wafanya kazi ,
UWT
Mkoa imewahamasisha kuingia kwenye ujasiliamali huo na wanaume wengi
wamekuwa Wakiwarudisha Nyuma kutokana na mizigo wanayo waachia ,
niwaombe wanaume kuepukana na fikra mgando ya kuwanyanyasa wanawake
pindi wanapo jishughulisha kwa kuwaachia kulea familia ,
Baba
ni kichwa katika familia wanatakiwa kutafuta fedha na kuwasaidia
wanawake kulea familia zao ilikuwasaidia watoto kupata elimu na malezi
bora", alisema Katibu wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa kigoma.


Baadhi ya akina mama wakijishughulisha na biashara zao mbalimbali za ujasiliamali mkoano Kigoma.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...