Na  Bashir  Yakub.

Tumesikia  mara  kadhaa  wazazi  wakigombania  kukaa  na mtoto/watoto. Haya  hujitokeza  baada  ya  kuvunjika  kwa  ndoa  kwa  talaka,  baada  ya  kutengana  bila  talaka   au  pasi  na  ndoa  wazazi  tu  wamezaa  na  sasa  hawaelewani  na  mgogoro  wa  nani  akae  na  mtoto  umeibuka.

Tunahitaji  kujua ikiwa kuna  haja  ya  kugombania  mtoto kwa matusi  na  ugomvi    wakati  zipo  taratibu  za  kisheria. Tujue  kama yafaa  kutumiana  jumbe  chafu  za  kudhalilishana pale   unapotaka  ukae  na  mtoto. Jibu  ni  hapana  ila  ni  watu  tu  wajue  taratibu.

Ifahamike  kuwa  iwe  kwa  ndoa  au  bila  ndoa   haki  ya  mtoto  kukaa  na  wazazi  au  mzazi   iko  kwa  yeyote. Ni  aidha  atakaa  na wote  wawili  au  mmoja  wao. Sheria  namba  21 ya  2009, Sheria  ya  Mtoto  ndiyo  sheria  ambayo  kwasasa  inasimamia  ustawi  na  haki  za  mtoto.  Hivyo  makala  yataeleza  yaliyo  katika  sheria  hii.

1.MTOTO  NI  NANI.
Kifungu  cha 4( a ) cha  sheria  ya  mtoto  kinatafsiri  neno  mtoto  kumaanisha  mtu  ambaye  yuko  chini  ya umri  wa  miaka  18. Kwa  maana  hii  miaka  18  kamili  sio  mtoto  isipokuwa sasa  chini  yake  ndiye  mtoto  kwa  tafsiri  ya  kifungu  hiki.

Sambamba na  hilo  kifungu  cha  7( 1 ) kinaeleza  haki  ya  mtoto  kukaa  na  wazazi  wake  wote  wawili. Basi  yaje  hayo   ya  kutengana   na  mtoto  kuishi  maisha ya  mzazi  mmoja , bado  uhalisia  ni  haki  ya  msingi   ya  mtoto  kukaa  na  wazazi  wake  wawili  kama  ilivyoainishwa  hapa.

KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...