Na EmanuelMadafa,Mbeya

Serikali Mkoani Mbeya imeahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya askari Polisi wanao tuhumiwa kuhusika na ubebaji wa mawe ya dhahabu katika shughuli za uokoaji wa wachimbaji waliofukiwa na kifusi mwezi February mwaka huu Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Hatua hiyo inakuja kufuatia baadhi ya wachimbaji madini wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Itumbi Kata ya Matundas Wilayani Chunya kutoa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla, ambaye alifika katika eneo hilo kujionea hali halisi ya maafa hayo, ambapo inaelezwa kuwa zaidi ya wachimbaji wadogo 25 katika mgodi wa dhahabu wa Itumbi,walifukiwa na kifusi na kusababisha majeruhi na vifo vya watu wanne, mwezi February mwaka huu.

Wachimbaji hao walidai mbele ya Mkuu wa Mkoa kuwa baadhi ya askari polisi ,walishindwa kutekeleza wajibu wao katika kufanya kazi ya uokoaji wa watu na mali zao, badala yake wao walikimbilia kubeba mawe ya dhahabu ambayo yalikuwa tayari yamechimbwa na wachimbaji hao, kisha kuyapakia kwenye gari ya polisi na kuyasafirisha mahala pasipojulikana.

Wachimbaji hao, walimweleza Makalla kuwa askari hao ambao wanadaiwa kuwa si waadilifu, wao waliendelea na shughuli ya ubebaji wa mawe ya dhahabu ambayo yalikuwa yamechimbwa na wachimbaji na yapo nje yakisubili kuchenjuliwa ili kupatikana madini aina ya dhahabu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na wachimbaji wadogo wadogo katika mgodi wa dhabau wa Itumbi kata ya Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya Februry 2 mwaka huu. 
Wachimbaji wadogo wadogo katika mgodi wa Itumbi kata ya Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji cha Itumbi Kata ya Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya February 2 mwaka huu. 
Mkutano ukiendelea. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...